WHO yaongeza uungaji mkono wakati mlipuko mpya wa Ebola ukilikumba Jimbo la Kasai nchini DRC

(CRI Online) Septemba 11, 2025

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza jana Jumatano kuwa linaendelea na juhudi zake za kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola, kufuatia nchi hiyo kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo katika Jimbo la Kasai.

Ndani ya saa 48 baada ya tangazo hilo lililotolewa Septemba 4, WHO imeshasafirisha kwa ndege tani 12 za nyenzo, vikiwemo vifaa vya kujikinga, nyenzo za kutenga wagonjwa, maji, dawa za kuua virusi, na vifaa vya usafi ili kuunga mkono huduma za kliniki na kulinda wahudumu wa afya wa mstari wa mbele.

Shirika hilo limeeleza kuwa, vifaa zaidi vinasafirishwa hadi nchini humo ili kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

"Maeneo yaliyoathiriwa ni vigumu kufikiwa. Tunafanya kazi muda wote kupanua kwa haraka hatua za mwitikio ili kuhakikisha udhibiti mkubwa wa mlipuko kwa ajili ya kuzuia virusi visisambae zaidi na kuokoa maisha" Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Mohamed Janabi, amesema katika taarifa yake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha