Lugha Nyingine
Burundi yapongeza uungaji mkono wa China kwa dira yake ya maendeleo ya muda mrefu
Serikali ya Burundi imeipongeza China kwa uungaji wake mkono katika kusukuma mbele maendeleo ya Burundi, ikisema unachangia katika kufikiwa dira ya Burundi ya kuwa nchi yenye uchumi unaoibuka ifikapo mwaka 2040 na nchi iliyoendelea ifikapo 2060.
Pongezi hizo zimetolewa siku ya Jumanne na waziri msaidizi wa mambo ya nje, mafungamano ya kikanda na ushirikiano wa maendeleo wa Burundi, Syldie Manirerekana, katika sherehe za kuadhimisha miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.
Hafla hiyo iliyofanyika katika ubalozi wa China mjini Bujumbura, ilihudhuriwa na Mke wa Rais wa Burudni Angeline Ndayishimiye, maafisa waandamizi wa serikali, wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao nchini Burundi, na Wachina wanaoishi nchini humo.
Bw. Syldie Manirerekana ameelezea baadhi ya mafanikio makubwa ya ushirikiano kati ya Burundi na China yakiwemo ujenzi wa ikulu ya Ntare House, kituo cha majaribio cha utafiti wa kilimo kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa usalama wa chakula, bwawa la kuzalisha umeme kwa maji la Ruzibazi, hospitali ya mkoa wa Mpanda, chuo cha mafunzo ya ualimu na chuo cha ufundi stadi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



