

Lugha Nyingine
Maonyesho ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China yamalizika kwa mafanikio ya kusainiwa kwa makubaliano yenye thamani ya yuan bilioni 644
Picha hii iliyopigwa Septemba 8, 2025 ikionyesha mwonekano wa nje wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Xiamen, ukumbi mkuu wa Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China, mjini Xiamen, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China. (Xinhua/Wei Peiquan)
XIAMEN - Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China (CIFIT) yamemalizika rasmi jana Alhamisi, yakifanikiwa kusaini makubaliano ya miradi 1,154 ya uwekezaji wenye thamani ya yuan bilioni 644 (dola za Kimarekani karibu bilioni 90.66), kamati ya maandalizi ya maonyesho hayo imesema.
Maonyesho hayo, ni maonyesho pekee ya China ya ngazi ya kitaifa yanayolenga kuhimiza uwekezaji. Maonyesho ya mwaka huu yalifanyika katika mji wa pwani wa Xiamen, mashariki mwa China kuanzia Septemba 8 hadi 11, ambapo zilifanyika shughuli 100 za uwekezaji.
Eneo la jumla la maonyesho hayo lilifikia mita za mraba 120,000, na maonesho yalivutia wageni kutoka nchi na maeneo zaidi ya 120 duniani. Mada tatu za maonesho hayo yanahusu: "Wekeza nchini China," "Uwekezaji wa China" na "Uwekezaji wa Kimataifa."
Yakiwa ni jukwaa muhimu la kuhimiza uwekezaji kati ya China na nchi mbalimbali duniani, Maonyesho hayo yalihusisha mazungimzo na makampuni makubwa ya kimataifa, kampuni zenye nguvu za kibinafsi na kampuni 500 Bora Duniani, na shughuli zaidi ya 30 za uwekezaji maalum, zikionyesha fursa na nguvu ya uwekezaji nchini China.
Wakati wa maonyesho hayo ya mwaka huu, ripoti 21 zilitolewa na wizara za China, mashirika ya kimataifa na mashirikisho ya wafanyabiashara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma