

Lugha Nyingine
China yatangaza miradi 10 ya majaribio kuhusu mageuzi ya ugawaji mambo ya uzalishaji kulingana na soko
BEIJING - Baraza la Serikali ya China limeidhinisha miradi 10 ya majaribio ya mageuzi ya kina kuhusu ugawaji wa mambo ya uzalishaji kulingana na soko ambapo mpango huo, utakapoanza kutekelezwa mara moja na kudumu kwa miaka miwili, unakuja huku kukiwa na juhudi kubwa za nchi hiyo kuhimiza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora, kusukuma mbele ujenzi wa soko la kitaifa lenye kigezo kimoja, na kujenga uchumi wa soko wa kijamaa wenye kiwango cha juu.
Mageuzi hayo yamepangwa kufanywa katika miji mikubwa kama vile Zhengzhou, Chongqing na Chengdu na pia katika maeneo maalum ya Beijing na mikoa kadhaa, ikiwemo Jiangsu, Zhejiang, Anhui, Fujian, Hunan, na Guangdong.
Katika maeneo hayo ya majaribio, jitihada zitafanywa ili kuondoa vizuizi vya kitaasisi vinavyozuia mtiririko huru na ugawaji bora wa mambo ya uzalishaji, na kuhakikisha kuwa wadau wa kiuchumi chini ya aina zote za umiliki wanakuwa na ufikiaji sawa wa mambo hayo ya uzalishaji, ushiriki wa haki katika ushindani wa soko, na ulinzi sawa wa kisheria.
"Maeneo hayo ya majaribio yatabeba jukumu la kuwa watangulizi, wa kupigiwa mfano katika kushughulikia changamoto katika mambo ya sasa ya soko, na yataweka misingi ya kutafuta uzoefu ambao unaweza kuigwa na kutekelezwa katika maeneo mengine," Li Chunlin, naibu mkurugenzi wa Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kufuatia kutangazwa kwa mpango huo.
Ameongeza kuwa, mageuzi hayo pia yatawezesha uchumi wa maeneo husika kwa kuimarisha usambazaji wa mambo hayo ya uzalishaji, na kwa kuchochea msukumo wa ndani na ustawi wa kivumbuzi.
China imekuwa ikifanya kazi kuhimiza ugawaji wa mambo ya uzalishaji kulingana na soko, ikijumuisha mambo ya jadi kama vile ardhi, kazi na mtaji, wakati huohuo ikiharakisha maendeleo ya teknolojia na masoko ya mambo ya data.
Mwezi Aprili 2020, China ilitoa mwongozo wa kuboresha ugawaji wa mambo ya uzalishaji kulingana na soko. Mwezi Januari 2022, ilitoa waraka uliokuwa ukielezea dira hadi mwaka 2025 ili kuzidisha mageuzi katika suala hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma