

Lugha Nyingine
Jeshi la Sudan lasema limeukamata tena mji wa kimkakati wa Bara katikati mwa nchi hiyo
(CRI Online) Septemba 12, 2025
Jeshi la Sudan limesema, limechukua udhibiti wa mji wa kimkakati wa Bara ulioko Jimbo la Kordofan Kaskazini baada ya miezi ya mapigano na wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF).
Chanzo cha kijeshi kimeliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwa sharti la kutotajwa, kwamba jeshi hilo lilizingira mji huo kwa siku kadhaa, na kudhoofisha mipaka ya ulinzi ya RSF na kukata mahitaji, na hatimaye kulazimisha wapiganaji wa RSF kuondoka mjini humo.
Bara ni kituo cha kimkakati katika barabara inayounganisha mji mkuu wa jimbo hilo la Kordofan Kaskazini, El Obeid, na barabara nyingine muhimu katika eneo hilo.
Kikosi cha RSF bado hakijatoa tamko lolote juu ya suala hilo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma