Rwanda yapongeza mchango wa China katika kuchochea maendeleo ya taifa

(CRI Online) Septemba 12, 2025

Waziri wa Nchi wa Rwanda anayeshughulikia mafungamano ya kikanda katika wizara ya mambo ya nje ya Rwanda Bw. James Kabarebe, amesema Rwanda inathamini ushiriki wa China katika sekta muhimu za maendeleo ya taifa la Rwanda.

Akiongea mjini Kigali katika hafla iliyofanyika kabla ya maadhimisho ya miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Kabarebe amesema uhusiano kati ya nchi hizo mbili umejengwa katika msingi wa kuaminiana, kuheshimiana na ushirikiano wa kivitendo, huku akisisitiza tena uungaji mkono wa Rwanda kwa sera ya kuwepo kwa China moja.

Amebainisha kuwa ushirikiano wa pande mbili katika sekta za miundombinu, afya, elimu na kilimo umetoa mchango mkubwa katika njia ya Rwanda kuelekea ukuaji wa taifa wa muda mrefu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha