Kenya yasisitiza kutetea jitihada za amani katika kusuluhisha migogoro

(CRI Online) Septemba 12, 2025

Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Kenya Bw. Musalia Mudavadi, amesema Kenya kuwa itaendelea kuweka kipaumbele katika ushirikiano wa kikanda na kuhimiza mazungumzo na njia za amani katika kutatua migogoro.

Bw. Mudavadi amesema Kenya ambayo imekuwa ikiongoza juhudi za amani katika eneo la Pembe ya Afrika na Ukanda wa Maziwa Makuu, bado inabaki kuwa na dhamira ya ushirikiano katika kuendeleza amani na usalama wa kikanda na kimataifa.

Akihutubia wanadiplomasia wa kigeni na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa mjini Nairobi, Bw. Mudavadi amesema Kenya itaendelea kuwa na msimamo thabiti kwa sheria za kimataifa, kanuni zilizowekwa, na utaratibu wa pande nyingi unaoheshimu kanuni.

Bw. Mudavadi ambaye pia anashughulikia mambo ya nje na diaspora ya nchi hiyo, amesema msukosuko wa sasa wa kimataifa unatoa wito wa mafungamano ya kikanda na ushirikiano mkubwa wa pande nyingi, katika kushughulikia changamoto mbalimbali, zikiwemo za matishio endelevu kwa amani na usalama, majanga matatu ya dunia, na dharura za kibinadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha