

Lugha Nyingine
Umoja wa Afrika walaani ukatili dhidi ya raia mashariki mwa DRC
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Bw. Mahmoud Ali Youssouf amelaani shambulizi la kinyama dhidi ya raia katika Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Watu takriban 80 wameuawa nyakati za usiku wa kuamkia Jumatatu hadi Jumanne kwenye kijiji cha Ntoyo katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF), mamlaka nchini humo zimelithibitishia Shirika la Habari la China, Xinhua.
Katika taarifa iliyotolewa mwishoni mwa Jumatano wiki hii, kiongozi huyo wa umoja huo ameelezea "mshtuko mkubwa" kuhusu shambulizi hilo baya.
“Mwenyekiti amelaani vikali shambulizi hilo baya la kigaidi, vilevile ghasia zinazotokea mara kwa mara ambazo zinaendelea kulenga raia mashariki mwa DRC” taarifa hiyo ya AU inasomeka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma