

Lugha Nyingine
Maonesho ya Biashara ya Huduma ya China yafungwa na kufikia Makubaliano 900, Yafuatilia Uvumbuzi wa Kidijitali
Mtembeleaji akionesha stempu alizozikusanya wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China 2025 (CIFTIS) katika Bustani ya Shougang mjini Beijing, China, Septemba 14, 2025. (Xinhua/Chang Nengjia)
BEIJING -- Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China (CIFTIS) ya mwaka 2025 yalifungwa Jumapili mjini Beijing yakisainiwa kwa makubaliano 900 yanayohusu sekta za ujenzi, teknolojia ya upashanaji habari na mambo ya fedha, yakionyesha ushiriki mkubwa wa kimataifa na uvumbuzi katika biashara ya kidigitali.
Maonesho hayo yaliyofanyika katika Bustani ya Shougang ya Beijing yaliwavutia washiriki kutoka zaidi ya nchi 60 na zaidi ya mashirika 20 ya kimataifa. Kampuni zilizo kwenye orodha ya Fortune Global 500, kampuni chipukizi (unicorns), na viwanda vinavyoongoza kwenye sekta husika vimeonesha mafanikio yao 198 katika sekta za AI, teknolojia za mambo ya fedha, huduma za afya na teknolojia ya kijani.
"Tutaendelea kutumia vizuri nafasi ya CIFTIS kama jukwaa la kukuza maendeleo, kupanua ufunguaji mlango na kuhimiza ushirikiano katika uvumbuzi, kuhakikisha matokeo na makubaliano yaliyofikiwa katika maonesho ya mwaka huu yanabadilishwa kuwa matokeo halisi,” alisema Zhu Guangyao, ofisa kutoka Kitengo cha Biashara ya Huduma na Huduma za Kibiashara cha Wizara ya Biashara ya China.
Zaidi ya mikutano 8,500 ya kibiashara ilifanyika kupitia jukwaa la kidijitali la ulinganishaji wa biashara la maonesho hayo, huku idadi ya wataalamu walioshiriki kwenye maonesho hayo imefikia 116,000, ikiongezeka kwa asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Maonesho hayo ya siku tano yalivutia zaidi ya watembeleaji 250,000 na yaliwashirikisha takribani waonyeshaji 5,600 wa mtandaoni. Ushiriki wa kimataifa umepanuka zaidi, na wafanyabiashara washiriki wa maonesho hayo wametoka nchi na maeneo 26 vilivyoko kwenye nafasi 30 zinazoongoza biashara ya huduma duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma