

Lugha Nyingine
China na Marekani zaanza Mazungumzo kuhusu Uchumi na Biashara huko Madrid, Hispania
Naibu waziri mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akipiga picha pamoja na Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent kabla ya mazungumzo yao huko Madrid, Hispania, Septemba 14, 2025. (Xinhua/Xing Guangli)
MADRID -- Wajumbe wa China na Marekani wamefanya mazungumzo kuhusu masuala ya uchumi na biashara Jumapili iliyopita huko Madrid, Hispnia.
Katika siku zijazo, pande hizo mbili zitajadili masuala kama vile hatua za Marekani za kutoza ushuru wa upande mmoja, matumizi mabaya ya udhibiti wa mauzo ya nje ya nchi, na suala la TikTok, msemaji wa Wizara ya Biashara ya China alisema Ijumaa.
Ujumbe wa China unaongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.
Msimamo wa China kuhusu suala la TikTok ni wazi na thabiti, msemaji huyo alisema. China inashikilia kulinda kwa uthabiti haki na maslahi halali ya kampuni zake na itashughulikia suala la TikTok kwa mujibu wa sheria na kanuni husika.
Wajumbe wa China na Marekani wamefanya mazungumzo kuhusu masuala ya uchumi na biashara huko Madrid, Uhispania, Septemba 14, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma