Maktaba iliyojengwa na Wachina chuoni UDSM yafungua Mlango Mpya kwa Wanafunzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2025

Picha iliyopigwa Septemba 9, 2025 ikionesha maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Picha iliyopigwa Septemba 9, 2025 ikionesha maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM -- Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambacho ni chuo kikuu kikubwa zaidi cha umma nchini Tanzania, maktaba iliyojengwa kwa msaada wa China inaboresha mazingira ya kusoma na kufanya utafiti kwa maelfu ya wanafunzi na wasomi.

Maktaba hiyo iliyozinduliwa rasmi Novemba 27, 2018 kwa msaada wa serikali ya China, imekua na kuwa moja ya vituo vikubwa zaidi na vya kiwango cha juu zaidi vya masomo katika Afrika Mashariki. Hivi leo, siyo tu kimekuwa kituo cha masomo bali pia kimekuwa kichocheo cha ushirikiano wa kimataifa.

Ikiwa na uwezo wa kuhudumia watu 2,500, maktaba hiyo ina mfumo wa intaneti ya kasi, upatikanaji wa kidigitali wa majarida ya duniani, na maabara ya kompyuta ya kisasa. Kwa wanafunzi wengi, maktaba hii siyo tu ni sehemu ya kusomea bali pia ni mazingira inayosaidia kufanya utafiti na kupata maendeleo ya taaluma.

Stanley Kulanga, mwenye umri wa miaka 32, mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) wa masomo kuhusu mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu, alisema maktaba hiyo ni muhimu kwa maendeleo yake ya kitaaluma.

"Tangu nilipoanza masomo yangu ya PhD, hii imekuwa mahali bora zaidi kwangu kujikita katika kusoma na kupata data ninazohitaji," Kulanga alisema katika mahojiano. "Kwa kawaida mimi huwa wa kwanza kuingia na wa mwisho kuondoka.”

Kwa wanafunzi kama Kulanga, maktaba hiyo inasimama kama alama ya fursa na pia ni alama ya uhusiano unaozidi kuimarika kati ya Tanzania na China.

Maktaba hiyo inaonesha ushirikiano unaozidi kwa kina zaidi, na idadi inayoongezeka ya Watanzania wanafukuzia masomo ya kiwango cha juu nchini China kwa ufadhili wa kiserikali, alisema Kelefa Mwantimwa, mkurugenzi wa huduma za maktaba wa chuo kikuu hicho.

Wanafunzi wakiwa kwenye maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wanafunzi wakiwa kwenye maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Mwanafunzi akisoma kitabu kwenye maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Mwanafunzi akisoma kitabu kwenye maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wanafunzi wakiwa kwenye maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 9, 2025.

Wanafunzi wakiwa kwenye maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Wanafunzi wakiwa kwenye maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 9, 2025.

Wanafunzi wakiwa kwenye maktaba iliyojengwa na Wachina katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha