

Lugha Nyingine
Namibia na China zasherehekea miaka 35 tangu kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati yao
Shughuli za kusherehekea miaka 35 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Namibia na China, sambamba na maadhimisho ya miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, zimefanyika Ijumaa iliyopita katika mji mkuu wa Namibia, Windhoek.
Katika taarifa yake, Naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Biashara wa Namibia Jenelly Matundu, kwa niaba ya Waziri husika, ametoa pongeza za dhati kwa China, akisisitiza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili una mizizi ya kina katika mshikamano, kuheshimiana na malengo ya pamoja.
Balozi wa China nchini Namibia Zhao Weiping amesema China imetoa msamaha kwa ushuru wa forodha kwa bidhaa za Namibia, hatua itakayotoa fursa mpya ya biashara kwa bidhaa za Namibia kama vile nyama ya kondoo, nyama ya mbuzi, na uvuvi.
Pia amezitaka nchi hizo mbili, kama wanachama wa Dunia ya Kusini, kushirikiana katika jukwaa la kimataifa, na kutetea mfumo wa kimataifa wenye usawa na haki zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma