

Lugha Nyingine
Serikali ya Sudan yaripoti mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye vituo muhimu vya kiraia nchini humo
(CRI Online) Septemba 15, 2025
Serikali ya Sudan imesema, vituo muhimu vya kiraia katika jimbo la kati la White Nile vimeshambuliwa jana na ndege zisizo na rubani za kundi la RSF.
Katika taarifa yake, Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan limesema, kundi la RSF lilitumia ndege zisizo na rubani kuharibu kituo cha umeme, ghala la mafuta na uwanja wa ndege wa kiraia wa Kenana katika jimbo la White Nile, na kuongeza kuwa, mashambulizi ya kundi hilo kwenye miundombinu ya kiraia ni "uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu."
Mpaka sasa, kundi la RSF halijatoa kauli yoyote kuhusu mashambulizi hayo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma