DRC yazindua kampeni ya chanjo ya Ebola mkoani Kasai

(CRI Online) Septemba 15, 2025

(Picha na Joel Lumbala/WHO/Ilichapishwa na Xinhua)

(Picha na Joel Lumbala/WHO/Ilichapishwa na Xinhua)

Jamhuri ya Kidemokraisa ya Kongo (DRC) imezindua kampeni ya chanjo ya Ebola katika eneo la Bulape, katikati ya nchi hiyo ambako mlipuko wa ugonjwa huo ulitangazwa mapema mwezi huu.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema, awamu inayoendelea ya utoaji wa chanjo inalenga wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele na watu waliowasiliana kwa karibu na wagonjwa waliothibitika kuwa na maambukizi ya Ebola.

Kwa mujibu wa WHO, awamu ya kwanza ya dozi 400 za chanjo ya Ervebo, ambayo inakinga spishi ya virusi vya Ebola aina ya Zaire, tayari imewasili Bulape, moja ya vitovu vya mlipuko huo katika mkoa wa Kasai, na dozi za ziara 45,000 zinatarajiwa kupelekwa eneo hilo katika siku zijazo.

Alhamis iliyopita, Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa Afrika (Africa CDC) kilisema, kesi 68 zinazoshukiwa kuwa na virusi hivyo zimeripotiwa, ikiwemo vifo 16.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha