

Lugha Nyingine
China na Marekani zafanya Mazungumzo ya Dhati na ya Kiujenzi kuhusu Biashara na TikTok
Li Chenggang (katikati), mjumbe wa biashara ya kimataifa wa China wa Wizara ya Biashara ambaye pia ni naibu waziri wa biashara, pamoja na Wang Jingtao (kulia), naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Usimamizi wa Mtandao wa Intaneti ya China, wakishiriki kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioendeshwa na msemaji wa Wizara ya Biashara He Yadong huko Madrid, Hispania, Septemba 15, 2025. (Xinhua/Xing Guangli)
MADRID -- Wajumbe wa China na Marekani wamebadilishana mawazo kwa dhati, kina na kiujenzi kwenye msingi wa kuheshimiana na kushauriana kwa usawa kuhusu masuala ya uchumi na biashara yanayofuatiliwa nao pamoja, yakiwemo ya TikTok, ofisa mwandamizi wa China alisema jana Jumatatu.
Pande hizo mbili zilitambua vya kutosha umuhimu mkubwa wa uhusiano tulivu wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani kwa nchi zote mbili na pia utaleta ushawishi mkubwa kwa utulivu na maendeleo ya uchumi wa dunia, alisema Li Chenggang, mjumbe wa biashara ya kimataifa wa China wa Wizara ya Biashara na Naibu Waziri wa Biashara, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
China na Marekani zikiwa nchi kubwa mbili zenye viwango tofauti vya maendeleo na mifumo tofauti ya uchumi, ni jambo la kawaida kwa nchi hizo kuwa na mizozo na migongano katika mchakato wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, alisema Li, akisisitiza kuwa muhimu zaidi ni kila upande unaheshimu maslahi makuu na ufuatiliaji mkubwa wa upande mwingine, na kupata njia mwafaka ya kutatua masuala kwa kupitia mazungumzo na mashauriano.
Kuhusu suala la TikTok, Li alisema China siku zote imekuwa ikipinga kuyafanya mambo ya teknolojia, uchumi na biashara yawe ya kisiasa, au kuwa vyombo na silaha, na kamwe haitaweza kufikia makubaliano kwa kupoteza kanuni, maslahi ya kampuni au usawa na haki za kimataifa.
Li amesema, China italinda kwa uthabiti maslahi ya nchi, haki na maslahi halali ya kampuni za China, na itatoa vibali vya kuuza teknolojia nje kwa kufuata sheria na kanuni husika, na serikali ya China pia inaheshimu nia ya kampuni na kuyaunga mkono kufanya mazungumzo ya kibiashara kwa usawa kwa kufuata kanuni za soko.
Li alisema, kwenye mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimejadili kwa dhati na kina kuhusu suala la TikTok na ufuatiliaji husika wa upande wa China, na zimefikia kimsingi maoni ya pamoja kuhusu kushughulikia masuala yanayohusu TikTok kwa kupitia ushirikiano, kupunguza vizuizi vya uwekezaji na kuhimiza ushirikiano husika wa kiuchumi na kibiashara.
Pande zote mbili zitaendelea kudumisha mawasiliano ya karibu, kujadili kwa umakini nyaraka za matokeo husika, na kila upande utahimiza kazi hii kwa kufuata utaratibu wa nchi yake wa kutolewa kwa idhani, Li aliongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma