

Lugha Nyingine
China yafanikiwa kufanya majaribio ya Mfumo wa Kusukuma Mbele wa Daraja la Kwanza wa Roketi ya Tianlong-3
Picha hii iliyopigwa Septemba 15, 2025, ikionyesha majaribio ya mfumo wa kusukuma mbele wa daraja la kwanza wa roketi inayotumia nishati ya kimiminika ya Tianlong-3, yaliyofanywa kwenye jukwaa la kurushia kwenye eneo la baharini katika Bandari ya Anga za Juu ya Haiyang Oriental, mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. (Xinhua)
Majaribio ya mfumo wa kusukuma mbele wa Daraja la kwanza wa roketi kubwa inayotumia nishati ya kimiminika ya Tianlong-3 yalifanyika kwa mafanikio mkoani Shandong siku ya Jumatatu.
Uhuishaji wa kujitegemea wa roketi ya Tianlong-3 ulianzishwa Machi 2022 na kampuni ya usafiri wa anga ya juu ya kibiashara ya China, Space Pioneer. Roketi hiyo ina urefu wa mita 72 na uzito wa tani 600 kwa kuanza kurushwa. Ina uwezo wa kurusha satelaiti 36 katika utekelezaji wa jukumu wa mara moja, na kusaidia usafirishaji wa mizigo mikubwa kwa kituo cha anga za juu cha China, pamoja na kurusha satelaiti hadi kwenye obiti ya kati na ya juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma