Mkutano Mkuu wa IAEA watoa wito wa kulinda mfumo wa kimataifa wa kutoeneza silaha za nyuklia

(CRI Online) Septemba 16, 2025

Mkutano Mkuu wa 69 wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) umefanyika jana mjini Vienna, Austria, na kutoa wito wa matumizi ya amani ya nishati na teknolojia ya nyuklia, na kulinda kwa pamoja mfumo wa kimataifa wa kutoeneza silaha za nyuklia.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi amesema, mkutano huo unafanyika katika wakati muhimu, huku kukiwa na ongezeko la pengo kati ya matajiri na maskini, ugaidi, migogoro mingi ya kijeshi, na mmomonyoko wa kanuni za nyuklia.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Nishati ya Atomiki ya China Bw. Shan Zhongde amesema, China inapenda kufanya kazi na IAEA na nchi nyingine ili kukuza usimamizi wa kimataifa wa nishati ya nyuklia uwe haki zaidi, yenye maendeleo shirikishi zaidi, na ushirikiano wa wazi zaidi na wenye utaratibu, ili kujenga vizuri zaidi jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha