

Lugha Nyingine
Faida za viwanda vikubwa vya China zarejea kuongezeka katika miezi minane ya kwanza
Mfanyakazi akiwa na pilika nyingi kwenye mstari wa uzalishaji ndani ya kampuni moja katika Mji wa Zunhua, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China, Septemba 27, 2025. (Picha na Liu Mancang/Xinhua)
BEIJING - Faida za viwanda vikubwa vya China ziliongezeka kwa asilimia 0.9 katika miezi minane ya kwanza ya mwaka 2025 kuliko mwaka jana wakati kama huo, ikibadilisha mwelekeo wa kushuka wa asilimia 1.7 katika kipindi cha Januari hadi Julai, takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) jana Jumamosi zimeonesha.
"Ukuaji huu unamaanisha kumaliza kwa mwenendo wa kushuka ambao umekuwa ukiendelea tangu Mei mwaka huu," amesema mwanatakwimu wa NBS Yu Weining, akihusisha mafanikio hayo na utekelezaji wa sera kuu, upigaji hatua katika kujenga soko la taifa lenye taratibu sawa, na kushuka kwa msingi wa ulinganifu kutoka mwaka mmoja uliopita.
Viwanda vikubwa, au kampuni zenye mapato ya biashara kuu ya mwaka ya angalau yuan milioni 20 (dola za Kimarekani kama milioni 2.81), zimeshuhudia faida zao za jumla za yuan karibu trilioni 4.7 katika kipindi cha miezi minane, NBS imeeleza.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, mwezi Agosti, faida za kampuni kubwa za kiviwanda zilirejea kwa kasi, zikipanda kwa asilimia 20.4 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, ikilinganishwa na kushuka kwa asilimia 1.5 mwezi Julai huku mapato yao ya biashara yakiongezeka kwa asilimia 1.9, asilimia moja kwa kasi zaidi kuliko mwezi uliopita.
"Faida za kampuni zenye ukubwa wa aina zote zilionyesha kuimarika, huku viwanda vya kutengeneza vifaa vikitoa uungaji mkono mkubwa," Yu amesema.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa, kuanzia Januari hadi Agosti, faida za kampuni kubwa ya kutengeneza vifaa ziliongezeka kwa asilimia 7.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo, ambazo ziliongeza faida ya jumla ya viwanda kwa asilimia 2.5.
Zinaonesha kuwa, faida iliongezeka katika sekta saba kati ya sekta nane za viwanda vya kutengeneza vifaa. Hasa, sekta za reli, ujenzi wa meli na anga zilishuhudia ongezeko la haraka la asilimia 37.3 ya faida, wakati ile ya mitambo ya umeme ilikua asilimia 11.5.
Ikisukumwa na ongezeko la mahitaji ya soko, kuimarika kwa bei na gharama zilizopunguzwa, faida za sekta ya viwanda vya kutengeneza malighafi zilipanda kwa asilimia 22.1 katika miezi minane ya kwanza, ongezeko la kasi la asilimia 10 kuliko kipindi cha Januari-Julai.
Akitaja mazingira magumu na yenye changamoto ya nje na kutosheleza kwa mahitaji ya soko la ndani, Yu amesema juhudi zaidi zinahitajika ili kupanua mahitaji ya ndani, kusukuma mbele ujenzi wa soko la taifa lenye taratibu sawa, na kutaratibu ushindani wa kibiashara ili kuweka mazingira mazuri zaidi kwa ajili ya uimarikaji endelevu wa faida ya viwanda.
Mfanyakazi akiwa na pilika nyingi kwenye mstari wa uzalishaji wa kampuni moja katika eneo maalum la viwanda mjini Lianyungang, Mkoani Jiangsu, mashariki mwa China, Septemba 27, 2025. (Picha na Geng Yuhe/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma