Rais Xi kutoa heshima kwa mashujaa wa taifa katika Siku ya Mashujaa

(CRI Online) Septemba 29, 2025

Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wa chama na serikali ya China wataweka mashada ya maua kwa mashujaa wa taifa waliofariki kwenye medani ya vita katika Uwanja wa Tian'anmen uliopo katikati mwa Beijing kesho Jumanne asubuhi, ili kuadhimisha Siku ya Kukumbuka Mashujaa.

Viongozi hao watajumuika na wawakilishi kutoka nyanja mbalimbali. Tukio hilo litatangazwa moja kwa moja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG).

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha