

Lugha Nyingine
Rais Xi ahimiza vyuo vya Chama kufanya kazi zaidi katika kuandaa vipaji na kutoa ushauri kwa CPC
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping katika maelekezo ya kazi za vyuo vya Chama (vyuo vya mambo ya utawala) jana Jumapili, amevihimiza vyuo vya Chama kufanya kazi zaidi katika kuandaa vipaji na kutoa ushauri kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesema kuwa tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC mwaka 2012, vyuo vya Chama katika ngazi zote vimekuwa vikiinua kiwango cha mafunzo na utafiti wao siku hadi siku, vikipata maendeleo na mafanikio mapya katika kazi zao.
"Vyuo vya Chama vinapaswa kushikilia utii kwa Chama na kukumbuka nia za kuanzishwa kwao," Rais Xi amesema, akivitaka vyuo hivyo kufanya elimu na mafunzo yao kuwa yenye kulenga mambo mahsusi na yenye ufanisi zaidi kupitia mageuzi, wakati huohuo vikiimarisha utafiti na ufafanuzi wa nadharia mpya za Chama.
Rais Xi pia amesisitiza umuhimu wa kuandaa makada na walimu wenye uwezo bora, kuboresha usimamizi na ufuatiliaji wa wanafunzi, na kuinua ubora wa uendeshaji wa vyuo vya Chama.
Maagizo hayo muhimu ya Rais Xi yaliwasilishwa na Chen Xi, Mkuu wa Chuo cha Chama cha Kamati Kuu ya CPC (Chuo cha Kitaifa cha Mambo ya Utawala), kwenye mkutano juu ya kazi ya vyuo vya Chama uliofanyika Beijing jana Jumapili.
Chen ametoa wito wa kufanya kazi kwa sifa bora ya hali ya juu katika kuandaa vipaji na kutoa ushauri, na amehimiza juhudi za kuboresha masomo ya nadharia mpya za Chama.
Chen Xi, Mkuu wa Chuo cha Chama cha Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (Chuo cha Kitaifa cha Mambo ya Utawala), akiwasilisha maelekezo muhimu ya Rais Xi Jinping wa China na kutoa hotuba kwenye mkutano juu ya kazi za vyuo vya Chama uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 28, 2025. (Xinhua/Shen Hong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma