Viongozi wa CPC wafanya mkutano kujadili masuala yanayohusu kuandaa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2025

BEIJING – Uamuzi uliotolewa kwenye mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulioongozwa na Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Rais wa China jana Jumatatu umeeleza kwamba, mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC utafanyika Beijing kuanzia Oktoba 20 hadi 23.

Mkutano huo umejadili masuala makubwa yanayohusu uandaaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) ya maendeleo ya uchumi na jamii.

Mkutano huo wa Ofisi ya Siasa umesikiliza ripoti kuhusu maoni yaliyokusanywa ndani na nje ya CPC kuhusu mapendekezo ya Kamati Kuu ya CPC ya kuandaa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano, na kuamua kuwa nyaraka hizo zitafanyiwa marekebisho kulingana na mjadala wa mkutano huo wa Jumatatu na kuwasilishwa kwenye mkutano huo ujao wa nne wa wajumbe wote.

Mkutano huo umesisitiza umuhimu wa kushikilia uongozi wa Chama kwa pande zote katika kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano na kutekeleza wazo la kutoa kipaumbele kwa watu ili kuhakikisha matunda ya ujenzi wa mambo ya kisasa yanaweza kuleta manufaa zaidi, kwa haki zaidi kwa wananchi wote. Mkutano huo umesisitiza maendeleo ya sifa bora ya hali ya juu, kuhimiza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora kulingana na hali halisi ya kila eneo husika, na kuendeleza mageuzi kwa kina na kwa pande zote, wakati huohuo kupanua ufunguaji mlango kwenye kiwango cha juu.

“China itahimiza maingiliano mazuri kati ya soko lenye ufanisi na serikali inayofanya kazi vizuri, kulifanya soko lifanye vya kutosha kazi ya uamuzi katika ugawaji rasilimali na kuhakikisha serikali ioneshe vizuri zaidi umuhimu wake ” mkutano huo umeeleza.

Mkutano huo pia umehimiza juhudi za kuhakikisha kazi za maendeleo na usalama zinaenda sambamba, na kuzuia na kupunguza hatari ipasavyo katika maeneo muhimu.

Mkutano huo umesema, "kushikilia na kuimarisha uongozi wa Chama katika pande zote ni hakikisho la kimsingi la kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, na ni lazima kusukuma mbele Chama kujiendesha kwa nidhamu kali kwa pande zote, na kuongeza uwezo wa uongozi wa Chama katika maendeleo ya uchumi na jamii. "

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha