Lugha Nyingine
Fuata Xi: Eneo Maalumu la Kiuchumi la Shenzhen Lasherehekea Miaka 45 ya kuanzishwa kwake, laendeleza "ujana" wake
Mwaka huu, Eneo Maalumu la Kiuchumi la Shenzhen, China linasherehekea maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwake. Eneo hilo, ambalo awali lilikuwa na mwanga wa mwenge wa wavuvi tu, leo hii linajaza mwanga angavu wa taa za maghorofa. Ukiwa na kasi ya ajabu ya "kujenga ghorofa moja kwa siku tatu", mji wa Shenzhen umekua kutoka kijiji cha wavuvi kisichojulikana hadi kuwa kituo cha uvumbuzi cha kimataifa, ukiandika maajabu ya sera ya mageuzi na kufungua mlango ya China.
Leo hii, hamasa ya kivumbuzi ya mji wa Shenzhen inaendelea kuongezeka, ukisonga mbele katika wimbi la maendeleo kwa kasi inayobadilika kila wakati. Mji wa Shenzhen ni muungaji mkono thabiti wa wajasilimali wanaotafuta fursa duniani, na mahali pa kuanzia kwa ndoto mbalimbali kukutana na kuanza safari pamoja. Shenzhen, inatoa jukwaa pana kwa kampuni nyingi kuanzishwa, kukua, na kupanua shughuli zao kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



