

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito wa kusonga mbele kwa kudhamiria katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu katika tafrija ya kuadhimisha miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 30, 2025. (Xinhua)
BEIJING – Rais wa China Xi Jinping wakati akitoa hotuba yake katika tafrija iliyofanyika Jumanne kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China kuadhimisha miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, ametoa wito kwa taifa hilo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kusonga mbele kwa kudhamiria katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Siku ya Taifa ya China iliadhimishwa jana Jumatano, Oktoba Mosi.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang aliongoza tafrija hiyo. Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria hafla hiyo pamoja na wageni wapatao 800 wa China na wa kigeni.
"Kufikia ustawishaji wa taifa la China ni kazi kubwa isiyo na kifani," Rais Xi amesema katika hotuba yake hiyo, akiongeza kuwa "vyote matarajio na changamoto vinatuhamasisha kutumia kikamilifu kila wakati na kustahimili mambo magumu kwa nguvu isiyoyumba."
Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesema kuwa miaka zaidi ya 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, CPC kimewaongoza watu kupata mafanikio makubwa kupitia moyo wa kujitegemea na jitihada za kila wakati.
"Si muda mrefu uliopita, China iliadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, ambayo imechochea uzalendo katika taifa zima na kuunganisha nguvu kwa ajili ya juhudi kubwa," Rais Xi amesema.
Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kujifunza kwenye uzoefu wa kihistoria ili kupata maendeleo makubwa zaidi ya taifa.
"Huku kukiwa na hali ngumu mwaka huu, China imepiga hatua mpya na kupata mafanikio katika kuendeleza kwa kina mageuzi kwa pande zote, kuhimiza maendeleo ya sifa bora, kuboresha ustawi wa watu, na kusukuma mbele kujisimamia kikamilifu na kwa nidhamu kali kwa Chama," Rais Xi amesema.
Akibainisha kuwa mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya CPC umepangwa kufanyika mwezi ujao ili kupitia kwa umakini mapendekezo kuhusu uundaji Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya taifa, Rais Xi amehimiza upangaji na utekelezaji mzuri wa malengo, majukumu na hatua za kimkakati za mpango huo wa miaka mitano ili kuhakikisha maendeleo ya lazima yanapatikana katika kutimiza kimsingi ujenzi wa mambo ya kisasa ya kijamaa.
Amesisitiza haja ya kutekeleza kwa uthabiti sera ya "nchi moja, mifumo miwili", na kuunga mkono mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Macao katika kufungamana vyema kwenye maendeleo ya jumla ya nchi, vilevile katika kukuza uchumi wao na kuboresha ustawi wa watu.
Jitihada zinapaswa kufanywa ili kuongeza kwa kina mabadilishano na ushirikiano katika Mlango-Bahari wa Taiwan, kupinga kithabiti shughuli za "Taiwan ijitenge" na uingiliaji wa nje, na kulinda kithabiti mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya taifa," Rais Xi amebainisha.
Wakati mabadiliko ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita yanatokea kwa kasi kubwa zaidi, "lazima tutekeleze ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kuhimiza utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo Duniani, Pendekezo la Usalama Duniani, Pendekezo la Ustaarabu Duniani na Pendekezo la Usimamizi Duniani, na kufanya kazi na nchi nyingine kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu," Rais Xi amesema.
Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Serikali ya China Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng, wakihudhuria tafrija ya kuadhimisha miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 30, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiongoza tafrija ya kuadhimisha miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 30, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma