AU na IGAD zalaani shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Somalia

(CRI Online) Oktoba 07, 2025

Umoja wa Afrika (AU) na Mamlaka ya Kiserikali juu ya Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) zimelaani shambulizi la kigaidi lililofanywa na kundi la al-Shabab lililolenga gereza moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili jioni, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf amelaani vikali shambulizi hilo dhidi ya gereza la Godka Jilicow, lililosababisha vifo na majeruhi ya watu kadhaa.

Katika taarifa nyingine, IGAD pia imelaani vikali shambulizi hilo, na kusifu vikosi vya usalama vya Somalia kwa mwitikio wa haraka na wa kimkakati uliowezesha kuokoa maisha ya watu.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Somalia imesema, Jumamosi iliyopita, vikosi vya usalama vya Somalia vilizuia shambulizi la kundi la al-Shabab dhidi ya gereza hilo, na kuua wapiganaji 7 wa kundi hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha