Meya wa Francistown nchini Botswana asifu mchango wa jamii ya Wachina

(CRI Online) Oktoba 07, 2025

Meya wa mji wa Francistown nchini Botswana, Gaone Majere amepongeza mchango wa jamii ya Wachina na timu ya madaktari wa China katika mji huo kwa mchango wao kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya wenyeji.

Akizungumza katika hafla ya kusherehekea Sikukuu ya Mbalamwezi iliyofanyika mjini humo siku ya Jumapili, Meya Majere amesifu jamii ya Wachina na wafanyabiashara kwa juhudi zao katika kushughulikia tatizo la ukosefu wa ajira kwenye mji huo.

Naye Balozi wa China nchini Botswana Fan Yong amesema, mwaka huu ni kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Botswana, na ushirikiano wa pande mbili umeendelea kuimarishwa katika sekta mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha