Kampuni ya China yaanza ujenzi wa bustani ya burudani nchini Ghana

(CRI Online) Oktoba 07, 2025

(Picha/CRI)

(Picha/CRI)

Hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bustani ya burudani inayojengwa na kampuni ya Greenhouse International Development Group ya China, imefanyika Jumamosi iliyopita mjini Afienya, nchini Ghana.

Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliyeweka jiwe hilo la msingi, amesifu wawekezaji wa China kwa kuendelea kuiamini Ghana kama kituo cha uwekezaji. Ameisifu kampuni hiyo kwa miradi yake tangu ilipoingia nchini Ghana mwaka 2011, ikiwemo Eneo Maalum la Viwanda la Bright International lenye viwanda kadhaa vinavyozalisha bidhaa za bei nafuu kwa Waghana, na kutoa ajira kwa wakazi wenyeji 10,000, na pia kwa uwekezaji wake katika sekta za kilimo na ujenzi.

Naye Mwenyekiti wa kampuni ya Greenhouse International Development Group Zheng Xiangming amesema, bustani hiyo itasimama kama hatua nyingine tena ya urafiki kati ya Ghana na China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha