Rais wa Madagascar ateua waziri mkuu mpya

(CRI Online) Oktoba 07, 2025

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina jana Jumatatu jioni amemteua Bw. Ruphin Fortunat Dimbisoa Zafisambo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, akichukua nafasi ya waziri mkuu Christian Ntsay aliyeondolewa madarakani hapo awali kufuatia maandamano yaliyoambatana na vurugu na uporaji mali katika mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo.

Rais Rajoelina amesisitiza kuwa, waziri mkuu huyo mpya lazima asaidie nchi "kurejesha utulivu" na kurejesha imani ya wananchi, huku kipaumbele cha kwanza kikiwa ni kutatua haraka masuala ya maji na upatikanaji wa umeme ambayo ndiyo yalikuwa chanzo cha maandamano hayo.

Kwa mujibu wa habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo, Bw. Zafisambo, mwanajeshi mkongwe, amekuwa akihudumu katika nafasi ya mkurugenzi wa ofisi ya kijeshi ya ofisi ya Waziri Mkuu tangu mwaka 2021.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha