

Lugha Nyingine
China yatoa wito kwa wanachama wa WTO kukabiliana pamoja na msukosuko wa biashara, na kushikilia mfumo wa pande nyingi
GENEVA - China imetoa wito kwa wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) kukabiliana pamoja na msukosuko wa biashara unaozidi kuwa mbaya siku hadi siku na kwa pamoja kushikilia maadili na kanuni za msingi za mfumo wa biashara wa pande nyingi.
Akizungumza chini ya kifungu cha ajenda ya "Msukosuko wa Biashara Unaozidi Kuwa Mbaya na Mwitikio wa WTO" iliyotolewa na China kwenye mkutano wa nne wa Baraza Kuu la WTO mwaka huu, uliofanyika kuanzia Jumatatu hadi Jumanne mjini Geneva, Uswizi, mjumbe wa kudumu wa China katika WTO Li Yongjie, amesema kuwa msukosuko wa uchumi na biashara duniani unaendelea na unazidi kuwa mbaya.
“Sera za biashara za Marekani zimevuruga minyororo ya usambazaji bidhaa na kuharibu masoko duniani, na kuwa chanzo kikuu cha kukosekana kwa utulivu duniani,” Li amesema, akiongeza kuwa baadhi ya pande wanachama zimelazimishwa kusaini makubaliano ya kuathiri haki na maslahi halali ya upande wa tatu.
Hii imesababisha uhusiano wa kibiashara wenye "msingi wa nguvu" ambao hatua kwa hatua unamomonyoa mfumo wa biashara wa pande nyingi wa kufuata "msingi wa sheria", Li amesema, akielezea ufuatiliaji mkubwa.
Li ametoa mapendekezo matatu katika kukabiliana na msukosuko wa biashara unaozidi kuwa mbaya, yakiwemo pamoja na kuimarisha hali wazi na uangalizi, kusisitiza pamoja ahadi na ufuataji wa mfumo wa biashara wa pande nyingi ulioanzishwa kwenye msingi wa kanuni, na kuchukua hatua madhubuti kuwezesha WTO kufikia matokeo ya kivitendo.
Umoja wa Ulaya (EU), Brazili, Australia, Uswizi, Pakistani, na pande wanachama wengine zimetoa wito wa kushikilia kanuni za kimsingi za WTO na kusukuma mbele mageuzi yake.
EU imeelezea ufuatiliaji mkubwa juu ya mmomonyoko wa mfumo wa biashara wa pande nyingi wenye "msingi wa kisheria" unaosababishwa na uhusiano wa biashara kwa "msingi wa nguvu".
Australia, New Zealand, Korea Kusini, na wanachama wengine zimetoa wito kwa Sekretarieti ya WTO kuimarisha usimamizi wa ushuru wa upande mmoja na makubaliano husika ya pande mbilimbili, kuhimiza wanachama kuijulisha WTO kuhusu makubaliano yao ya pande mbilimbili.
Nigeria na Bangladesh zimesisitiza athari za ushuru huo wa upande mmoja na hali ya kutokuwa na uhakika katika mazingira ya biashara kwa pande wanachama zinazoendelea zilizo za udhaifu, zikiihimiza WTO kutoa msaada wa lazima.
Pande wanachama zikiwemo Venezuela, Nicaragua, na Cuba zimelaani ushuru wa upande mmoja wa Marekani na mbinu zake za kulazimisha kwa nguvu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma