China na Italia zasisitiza kuimarisha uhusiano, na kuahidi ushirikiano wa karibu zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Italia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Antonio Tajani mjini Rome, Italia, Oktoba 8, 2025. (Xinhua/Li Jing)

ROMA - Historia ya mawasiliano kati ya China na Italia imeonyesha kwa kutosha kwamba kufungua mlango, ushirikiano, na kuendeleza kwa pamoja ni machaguo sahihi kulingana na urithi wa kitamaduni na mahitaji ya kivitendo ya nchi zote mbili, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema Jumatano alipokutana na Naibu Waziri Mkuu wa Italia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Antonio Tajani mjini Roma, Italia.

"Machaguo haya hutumikia maslahi ya kimsingi na ya muda mrefu ya pande zote mbili na kuonyesha matarajio ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili," amesema Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 55 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Italia, Wang amesema, akiongeza kuwa katika zaidi ya nusu karne iliyopita, nchi hizo mbili zimefanya ushirikiano wa ngazi ya juu na wa kivitendo, kuhimiza mawasiliano ya kiwango cha juu ya kitamaduni na ya kati ya watu, na kujenga ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wenye matunda.

“China inapenda kushirikiana na Italia kuimarisha hali ya kuaminiana, kuondoa uingiliaji, kutekeleza kwa juhudi zote mpango kazi wa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, kuhimiza mafanikio zaidi katika ushirikiano wa pande mbili na kuongeza maendeleo ya kiuchumi ya nchi hizo mbili” Wang ameongeza.

Wang amesema kuwa zikiwa washirika wa kimkakati wa pande zote, China na Italia zinapaswa kudumisha mazungumzo ya karibu, kuaminiana na kuungana mkono, na kushughulikia masuala makuu yanayofuatiliwa na kila upande. Amesema, China inatumai na inaamini kuwa Italia itaendelea kufuata kwa uaminifu kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuimarisha msingi wa kisiasa kwa ajili ya ukuaji mzuri na thabiti wa uhusiano wa pande mbili.

Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuendelea kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili kupitia hatua madhubuti, na kugeuza nia njema ya kisiasa kuwa chachu kwa ajili ya kuendeleza uhusiano kati ya China na Italia.

Kwa upande wake Tajani amesema, Italia inaweka umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wake na China na kwamba pande hizo mbili zimepata matokeo ya ajabu ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali ndani ya mfumokazi wa ushirikiano wa kimkakati na zimejenga uhusiano wa kiujenzi na wa kunufaishana.

Ameongeza kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara hutumika kama chachu muhimu kwa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili huku akieleza matumaini yake kuwa pande zote mbili zitaimarisha mazungumzo na mawasiliano kupitia mifumo ya pande mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Italia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Antonio Tajani mjini Rome, Italia, Oktoba 8, 2025. (Xinhua/Li Jing)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Italia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Antonio Tajani mjini Rome, Italia, Oktoba 8, 2025. (Xinhua/Li Jing)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na waandishi wa habari pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Italia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Antonio Tajani mjini Rome, Italia, Oktoba 8, 2025. (Xinhua/Li Jing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha