China yaunga mkono ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika

(CRI Online) Oktoba 09, 2025

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei amehutubia mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama kuhusu Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika Jumanne wiki hii, akisisitiza kuwa China inaunga mkono ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Balozi Sun amesema Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja huo zinapaswa kuunga mkono juhudi zinazoendelea za usuluhishi za Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kikanda, ili kutatua masuala ya bara hilo kwa njia ya Afrika.

Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu mamlaka na haki za nchi za Afrika, kuepuka uingiliaji na shinikizo wa nje, na matumizi mabaya ya vikwazo vya upande mmoja vya wadau wa nje, ili kuweka mazingira mwafaka kwa ajili ya utatuzi wa migogoro.

Pia amesisitiza kuwa China inaunga mkono mkono kithabiti Afrikakuonesha umuhimu mkubwa zaidi katika mambo ya kimataifa, na kuongeza uwakilishi na sauti ya Afrika katika mfumo wa pande nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha