Watu 12 wauawa katika shambulizi la makombora dhidi ya Hospitali ya El Fasher, Sudan

(CRI Online) Oktoba 09, 2025

Shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa Madaktari wa Sudan, limesema, watu 12 wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa, wakiwemo wahudumu wa afya, katika shambulizi la makombora linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) dhidi ya hospitali ya El Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana imesema, shambulizi hilo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, na ni sawa na "uhalifu wa kivita."

Mtandao huo umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na mashirika ya kibinadamu kuchukua hatua za haraka kukomesha mashambulizi ya RSF kwenye vituo vya matibabu, vituo vya huduma, na nyumba za raia, na kulinda mfumo wa afya wa El Fasher ambao kwa sasa uko katika hali mbaya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha