AfDB yasema Afrika inahitaji dola trilioni 1.3 za kimarekani kutimiza malengo ya maendeleo

(CRI Online) Oktoba 09, 2025

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema jana Jumatano kwamba Afrika inahitaji dola za kimarekani karibu trilioni 1.3 ili kuweza kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Afrika (ADF) unaofanyika Lusaka, mji mkuu wa Zambia, Rais wa Benki hiyo Sidi Ould Tah amesema, karibu nusu ya fedha hizo zinawakilisha pengo la ufadhili wa kifedha kutoka nje.

Amehimiza washirika wa maendeleo kufanya marekebisho ya mkataba wa ADF kabla ya mwisho wa mwaka, hatua itakayoruhusu mfuko huo kuzidi asilimia 85 ya ukomo wa mkopo.

Mkutano huo wa siku tatu umewakutanisha washirika wa maendeleo, nchi wapokeaji na uongozi wa AfDB kwa lengo la kutafuta njia ya ukuaji jumuishi, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, mafungamano ya kikanda, maendeleo ya sekta binafsi, na mageuzi katika uongozi barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha