Timu ya madaktari wa China yatoa huduma bila malipo ya kliniki Tanzania Zanzibar

(CRI Online) Oktoba 09, 2025

Kundi la 35 la timu ya madaktari wa China limetoa huduma bila malipo ya kliniki katika Bustani ya Mimea, Tanzania Zanzibar jana Jumatano, ambapo limetoa huduma kwa wakazi wa maeneo ya vijijini na maeneo yasiyofikiwa kwa urahisi.

Mkuu wa timu hiyo ya madaktari wa China Bao Zengtao amesema, shughuli hiyo ililenga kutoa huduma bora za afya moja kwa moja kwa wakazi wenyeji na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya, hususan kwa wanawake.

Katika shughuli hiyo, idara mbalimbali zilihusika, ikiwemo za masuala ya wanawake, meno, macho, matatizo ya tumbo, upasuaji, na magonjwa ya mfumo wa hewa.

Ofisa wa afya kutoka Wizara ya Afya ya Zanzibar, Maryam Hamdu Khalfan amesema, kliniki hiyo imepeleka huduma za kitaalamu za afya karibu na watu, na kuonyesha utaalamu, ufanyaji kazi kama timu, na moyo wa ubinadamu wa timu ya madaktari wa China nje ya nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha