

Lugha Nyingine
Mkuu wa IMF asema uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto halisi
(CRI Online) Oktoba 09, 2025
Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kristalina Georgieva, jana Jumatano mjini Washington ameonya kwamba uchumi wa dunia ni "bora kuliko ilivyokadiriwa, lakini mbaya kuliko tunavyohitaji." Aliongeza kuwa uhimilivu wa dunia bado haujajaribiwa kikamilifu, na kuna ishara za wasiwasi kwamba jaribu linaweza kuja.
Georgieva amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ikiwemo ya siasa za kijiografia, mapinduzi ya kiteknolojia, na muundo wa idadi ya watu, pamoja na uharibifu unaoongezeka kwa dunia unaofanywa na binadamu, mambo yanayosababisha sintofahamu.
"Hali ya kutokuwa na uhakika kiuchumi duniani itaendelea kuwa 'kawaida mpya'" alisema Georgieva.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma