

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma salamu za pongezi kwa Kiongozi wa DPRK Kim Jong Un kuadhimisha miaka 80 ya WPK
Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Kiongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu ya Korea (DPRK) ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Workers cha Korea (WPK) Kim Jong Un kwa kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
Rais Xi amesema katika kipindi cha miaka 80 iliyopita, WPK kimeungana na kuongoza watu wa DPRK kusonga mbele na kushinda matatizo, kikipata mafanikio makubwa katika kuhimiza mambo ya ujamaa ya DPRK.
Amesema katika miaka ya hivi karibuni, Kim amekiongoza Chama na watu katika kuimarisha kikamilifu ujenzi wa Chama, kuendeleza uchumi, na kuboresha maisha ya watu.
Ameelezea matumaini yake kuwa chini ya uongozi thabiti wa WPK ukiongozwa na Katibu Mkuu Kim Jong Un, malengo ya kijamaa ya DPRK yataendelea kupata mafanikio mapya, na pia ameutakia mafanikio mkutano mkuu wa tisa wa WPK.
Rais Xi pia amesema China itaendelea kufanya kazi na DPRK kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuzidisha ushirikiano wa kivitendo, kuongeza uratibu na kuhimiza maendeleo tulivu ya uhusiano wa pande mbili, ili kuhudumia vema ujenzi wa kijamaa wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango kwa amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kikanda na wa dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma