China ingependa kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na DPRK, asema Waziri Mkuu Li

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 10, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Workers cha Korea na Rais wa Masuala ya Nchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), mjini Pyongyang, DPRK, Oktoba 9, 2025. (Xinhuang/Jingwea)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Workers cha Korea (WPK) na Rais wa Masuala ya Nchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu ya Korea (DPRK), mjini Pyongyang, DPRK, Oktoba 9, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

PYONGYANG - Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Alhamisi kwenye mkutano wake na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Workers cha Korea (WPK) na Rais wa Masuala ya Nchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu ya Korea (DPRK) amesema kuwa China ingependa kuimarisha mabadilishano ya ngazi ya juu na mawasiliano ya kimkakati na DPRK.

Li ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amefikisha salamu za dhati na za kutakia kila la kheri za Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping kwa Katibu Mkuu Kim, vilevile pongezi zake za dhati kwa kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa WPK.

Li amebainisha kuwa mwezi uliopita, Katibu Mkuu Kim alikuja China kuhudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti ambapo wakati wa mkutano wake na Katibu Mkuu Xi, walibainisha mwelekeo na kuweka mpango wa kuendeleza kwa kina uhusiano kati ya China na DPRK.

"CPC na serikali ya China daima zimekuwa zikichukulia uhusiano na DPRK kutoka ngazi ya kimkakati na mtazamo wa muda mrefu," Li amesema, akiongeza kuwa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa jadi wa kirafiki na uhusiano wa kiushirika kati ya nchi hizo mbili ni sera isiyoyumba ya China.

Amesema, China ingependa kushirikiana na DPRK ili kufuata mwongozo wa pamoja wa viongozi wakuu wa vyama hivyo viwili na vilevile wa nchi hizo mbili, na kuhimiza upigaji hatua mpya katika uhusiano wa pande mbili.

Waziri Mkuu huyo wa China amesema China ingependa kufanya kazi na DPRK ili kusukuma mbele zaidi urafiki wao wa jadi, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kivitendo, na kuratibu na kushirikiana kwa ukaribu katika masuala ya kimataifa na kikanda.

Li pia ametoa wito kwa pande hizo mbili kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi, kithabiti kulinda na kutekeleza mfumo wa pande nyingi, na kuhimiza maendeleo ya utaratibu wa kimataifa katika mwelekeo wa haki na usawa zaidi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kim amemwomba Li afikishe salamu zake za dhati na za kutakia kila kheri kwa Katibu Mkuu Xi, na amekaribisha kwa moyo mkunjufu ujumbe wa chama na serikali wa China nchini DPRK kwa ajili ya maadhimisho hayo, akisema kuwa chini ya uongozi wa busara wa Katibu Mkuu Xi, China imepata mafanikio makubwa katika ujenzi wa mambo ya kijamaa.

Kim amesema, DPRK, inaunga mkono kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, inapinga kithabiti vitendo vya "Taiwan ijitenge" na uingiliaji wowote wa nje, na inaunga mkono msimamo wa China kuhusu masuala yanayohusiana na Hong Kong, Xinjiang na Xizang.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha