

Lugha Nyingine
Makamu Rais wa Zimbabwe apongeza eneo maalum la viwanda lililowekezwa na kampuni za China
HARARE - Makamu Rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga amepongeza eneo maalum la viwanda lililowekezwa na kampuni za China kwa kuongeza msukumo wa maendeleo ya viwanda na ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi hiyo.
Akifungua rasmi mkutano wa madini, uhandisi na usafiri mjini Bulawayo, Chiwenga amesema Eneo Maalum la Kiuchumi la Palm River Energy Metallurgiska lililowekezwa na kampuni za China ni mradi wa kimkakati ambao unaongeza uwezo wa kunufaika na madini wa nchi hiyo, usambazaji nishati na utoaji ajira.
Ukiwa ulizinduliwa na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mwezi Februari, Mradi huo ulio katika Jimbo la Matabeleland Kusini la Zimbabwe unajumuisha uzalishaji nishati na viwanda vya mambo ya metali. Utatekelezwa kwa awamu tano kwa muda wa miaka 12 ili kuzalisha nyenzo zinazotokana na chromium na coke.
"Tunapongeza uzinduzi wa hivi karibuni wa miradi ya kimkakati kama vile Kiwanda cha Metallurgical cha Palm River. Haya ni mafanikio ambayo yanaimarisha manufaa na kujitosheleza kwa nishati," Chiwenga amesema.
Chiwenga amesema Zimbabwe inasukuma kwa ajili ya manufaa zaidi ya ndani ya rasilimali za madini ili kuharakisha maendeleo ya viwanda na kuhimiza wachimbaji madini kwenda zaidi ya uchimbaji wa madini na kujumuisha manufaa na uongezaji thamani katika shughuli zao.
"Kwa wawekezaji, wote wa ndani na wa kimataifa, Zimbabwe bado iko wazi kwa biashara," amesema. "Tunatafuta ushirikiano wenye kunufaishana ambao unahakikisha madini chini ya ardhi yetu yanawawezesha watu wetu wote."
Uchimbaji madini unaendelea kuwa sekta muhimu ya uchumi wa Zimbabwe, ukichangia asilimia zaidi ya 70 katika mapato ya mauzo ya nje ya nchi hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma