

Lugha Nyingine
Wizara ya Biashara ya China yasema, hatua za China za kulipiza ada za bandari za Marekani ni "ulinzi halali"
BEIJING – Wizara ya Biashara ya China jana Ijumaa ilisema, hatua za China za kulipiza ada za nyongeza za bandari za Marekani kwa meli za China ni hatua za "kujilinda kihalali" zinazolenga kudumisha mazingira ya ushindani wa haki katika masoko ya kimataifa ya usafiri wa meli na uundaji meli.
"Hatua ya Marekani ni kitendo dhahiri cha upande mmoja chenye hali ya kubagua, ambayo inaathiri vibaya maslahi ya kampuni za China," msemaji wa wizara hiyo amesema katika taarifa ya mtandaoni.
Msemaji huyo amesema, ili kulinda maslahi ya viwanda vya ndani, mamlaka za China zikifuata sheria na kanuni za kimataifa, zitatoza ada maalum za bandari kwa meli zenye uhusiano na Marekani, zikiwemo zile zinazopeperusha bendera ya Marekani, zilizoundwa nchini Marekani, au zinazomilikiwa, kudhibitiwa au kuendeshwa na kampuni za Marekani.
"Hatua hizi za kulipiza zitaanza kutekelezwa kwa wakati mmoja na Marekani inapoanza kutoza ada za nyongeza za bandari kwa meli za China Oktoba 14. China inautaka upande wa Marekani kurekebisha makosa yake na kufanya mashauriano ya usawa na ushirikiano na China ili kutafuta mpango wa kutatua matatizo," msemaji huyo ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma