Naibu Waziri Mkuu wa China azitia moyo kampuni za kimataifa kupanua uwekezaji nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2025

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) jana hapa Beijing akikutana na viongozi wa kampuni kubwa tatu za kimataifa: Abbott Laboratories kutoka Marekani, Prudential kutoka Uingereza, na SK Group kutoka Jamhuri ya Korea.   (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING – Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng jana Ijumaa alipokutana na viongozi wa kampuni kubwa tatu za kimataifa: Abbott Laboratories kutoka Marekani, Prudential kutoka Uingereza, na SK Group kutoka Jamhuri ya Korea, mjini Beijing, amezitia moyo kampuni kubwa za kimataifa kupanua uwekezaji wao nchini China kwani China itaendelea kupanua ufunguaji mlango wake kwa vigezo vya juu.

He, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kwamba uchumi wa China una misingi imara, nguvu bora katika sekta nyingi, uhimilivu dhahiri na uwezo mkubwa ambao haujaonekana na pia amesisitiza kuwa mwelekeo mkuu wa kuongoza maendeleo mazuri ya muda mrefu ya uchumi wa China na hali mbalimbali zinazotegemewa kwa maendeleo hayo havijabadilika.

He amezitia moyo kampuni kubwa za kimataifa kupanua uwekezaji wao nchini China, kuendelea kwa kina ushirikiano na China ili kunufaika pamoja na fursa za maendeleo.

Viongozi wa kampuni hizo wameelezea matumaini yao kwa matarajio ya uchumi wa China, wakieleza nia yao ya kuimarisha uwepo wao katika soko la China na kupanua ushirikiano wao na China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha