Rais wa Uturuki aionya Israel dhidi ya kuvunja ahadi za kusimamisha mapigano Gaza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akitoa hotuba kwenye hafla ya kuzindua miradi mipya katika Jimbo la Bahari Nyeusi la Rize, Uturuki, Oktoba 10, 2025. (Mustafa Kaya/kupitia Xinhua)

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akitoa hotuba kwenye hafla ya kuzindua miradi mipya katika Jimbo la Bahari Nyeusi la Rize, Uturuki, Oktoba 10, 2025. (Mustafa Kaya/kupitia Xinhua)

ANKARA - Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan jana Ijumaa wakati akizindua miradi mipya katika Jimbo la Bahari Nyeusi la Rize, amesema kuwa ni muhimu kuizuia Israel isivunje ahadi za kusimamisha mapigano Gaza huku akikaribisha makubaliano yaliyotiwa saini nchini Misri kati ya Israel na Hamas.

"Makubaliano yametiwa saini na njia kuelekea amani ya kudumu huko Gaza imefunguliwa," Erdogan amesema, akiongeza kuwa "jambo la muhimu zaidi kwa sasa ni kuhakikisha kuwa makubaliano hayo yanatekelezwa kikamilifu."

Amesema Uturuki itachangia katika mchakato wa utekelezaji. "Tutawasilisha haraka Gaza msaada wa kibinadamu ulio kwenye meli zetu zinazosubiri katika bandari ya El-Arish ya Misri."

Ameishutumu Israel kwa kuvunja ahadi za awali za kusimamisha mapigano, akionya kwamba "kurudi katika mazingira ya mauaji ya kimbari kutakuwa na gharama kubwa."

"Tunajua rekodi mbaya ya Israel ya kuvunja ahadi zake... Pia tunajitahidi kuchukua hatua hitajika ili kuwazuia kuchukua njia ile ile mbaya kwa mara nyingine," Erdogan amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha