

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa mapendekezo ya kusukuma mbele maendeleo ya wanawake ya pande zote
Rais Xi Jinping wa China akihudhuria kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake na kutoa hotuba kuu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, Oktoba 13, 2025. (Xinhua/Shen Hong)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake mjini Beijing, ametoa mapendekezo manne ya kuharakisha mchakato wa maendeleo ya wanawake ya pande zote.
Rais Xi amesema mapendekezo hayo yametolewa ili kujenga maafikiano mapana zaidi, kufungua njia pana zaidi na kuchukua hatua zaidi za kivitendo kwa ajili ya mambo ya wanawake, kwani maendeleo ya wanawake ya pande zote bado yanakabiliwa na changamoto zenye utatanishi.
Rais huyo wa China amependekeza kufanya juhudi za pamoja za kujenga mazingira yanayosaidia ukuaji na maendeleo ya wanawake.
"Maendeleo ya wanawake ya pande zote yanafikiwa chini ya sharti la amani na utengamano," Rais Xi amesema.
Amesisitiza haja ya kuimarisha kazi ya kuwalinda wanawake na mabinti katika maeneo yaliyokumbwa na vita, migogoro, umaskini au maafa, na kuunga mkono wanawake kuonesha umuhimu wao katika kuepusha migogoro na kujenga upya maskani yao. "Ni muhimu sana kwa kukamilisha mifumo ya kuzuia unyanyasaji wa kimabavu na kupambana kithabiti na aina zote za ukatili dhidi ya wanawake," Rais Xi ameongeza.
Rais huyo amependekeza kujenga msukumo mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya sifa bora ya juu ya mambo ya wanawake.
Rais Xi amehimiza juhudi za kushughulikia hali isiyo ya uwiano na isiyo ya kutosha katika maendeleo ya wanawake duniani kote, na kuwezesha wanawake wote kunufaika pamoja na matunda ya utandawazi wa uchumi wa dunia.
“Ni muhimu kutumia ipasavyo uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia ili kusukuma mbele maendeleo ya sifa bora ya juu ya wanawake, na kuunga mkono wanawake katika kubeba jukumu kubwa zaidi katika maendeleo ya kijani” amesema.
Rais Xi pia amependekeza kuanzisha mfumo wa usimamizi ili kulinda haki na maslahi ya wanawake.
Ametoa wito wa kukamilisha mifumo na sheria, na kutoa sera na hatua zaidi halisi zinazoweza kupata matokeo, na kutoa rasilimali bora zaidi za afya na elimu kwa wanawake wote.
"Ni muhimu kujenga mazingira ya jamii yaliyo ya jumuishi na yenye mapatano ambayo yanawawezesha wanawake kukwepa athari ya ubaguzi na mitizamo ya kuwadhalilisha, kupanua njia za wanawake kushiriki na kuamua juu ya masuala ya kisiasa, na kuunga mkono ushiriki wao zaidi katika utawala wa nchi na na usimamizi wa jamii," amebainisha.
Rais Xi amesisitiza haja ya kujenga mazingira ya kuheshimu wanawake, na kubadilisha usawa wa jinsia kuwa kanuni za mienendo zinazofuatwa na kila mmoja katika jamii.
Rais huyo pia amependekeza kuandika ukurasa mpya katika kuhimiza ushirikiano wa wanawake wa kote duniani. Ametoa wito wa kuwaunga mkono wanawake waoneshe umuhimu wao halisi katika usimamizi wa dunia, na kunufaika pamoja na matokeo yake.
Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu na wajumbe wa nchi mbalimbali na wenzi wao wanaohudhuria Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake mjini Beijing, Oktoba 13, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
Rais Xi Jinping wa China akihudhuria kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake na kutoa hotuba kuu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, Oktoba 13, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
Rais Xi Jinping wa China akihudhuria kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake na kutoa hotuba kuu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China mjini Beijing, Oktoba 13, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma