Rais Xi akutana na Waziri Mkuu wa Msumbiji Maria Benvinda Delfina Levi mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2025

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Msumbiji Maria Benvinda Delfina Levi, ambaye alikuwa Beijing  kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing,  Oktoba 14, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Waziri Mkuu wa Msumbiji Maria Benvinda Delfina Levi jana Jummane, ambaye alikuwa Beijing kwa kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake ambapo amesema urafiki wa jadi kati ya China na Msumbiji umekuwa imara kama mwamba tangu nchi hizo mbili zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 50 iliyopita.

"China inapenda kuendeleza kwa kina hatua kwa hatua uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote na Msumbiji na kwa pamoja kuingia kwenye zama tukufu zaidi katika miaka 50 ijayo," Rais Xi amesema.

Amesisitiza uungaji mkono wa China kwa Msumbiji katika kutafuta kwa kujiamulia njia za maendeleo zinazolingana na hali halisi ya nchi yake na kulinda umoja na utulivu wa kitaifa.

"Pande hizo mbili zinapaswa kutafuta kwa pamoja njia mpya za maendeleo jumuishi na ukuaji wa uratibu katika rasilimali za nishati na madini na ujenzi wa miundombinu," Rais Xi amesema.

Rais Xi pia amesema China inapenda kushirikiana Msumbiji katika kutekeleza pamoja Pendekezo la Usimamizi wa Dunia, kupinga maamuzi ya upande mmoja na umwamba, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zote mbili na Nchi za Kusini mwa Dunia.

Kwa upande wake Levi amesema Msumbiji inapenda kushirikiana na China ili kutekeleza kwa pamoja matokeo ya Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake na kuhimiza mambo ya wanawake duniani.

"Msumbiji inatarajia kufanya ushirikiano kwa ukaribu na China katika sekta za uchumi, biashara, nishati, madini, sayansi na teknolojia na elimu," amesema Levi.

Levi amesema Msumbiji inathamini mchango wa China katika ustawi na utulivu duniani kwa maendeleo yake yenyewe, akiongeza kuwa Msumbiji itaimarisha ushirikiano na China chini ya mifumokazi ya pande nyingi na kufanya usimamizi wa dunia kuwa wa haki na usawa zaidi.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Msumbiji Maria Benvinda Delfina Levi, ambaye alikuwa Beijing kwa kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Duniani kuhusu Wanawake kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Oktoba 14, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha