Uzalishaji na Mauzo ya Magari yanayotumia Nishati Mpya ya China vyaongezeka katika miezi 9 ya kwanza ya 2025

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2025

Wateja wakitazama magari yanayotumia nishati mpya kwenye  duka lililoko Eneo la Wuchang la Mji wa Wuhan, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Oktoba 14, 2025. (Picha na Zhao Jun/Xinhua)

Wateja wakitazama magari yanayotumia nishati mpya kwenye duka lililoko Eneo la Wuchang la Mji wa Wuhan, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Oktoba 14, 2025. (Picha na Zhao Jun/Xinhua)

BEIJING - Sekta ya magari yanayotumia nishati mpya ya China (NEV) imedumisha mwelekeo wenye nguvu wa uzalishaji na mauzo katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2025, takwimu zilizotolewa jana Jumanne na Jumuiya ya Waundaji Magari ya China (CAAM) zinaonyesha.

Uzalishaji wa NEV uliongezeka kwa asilimia 35.2 na kufikia magari milioni 11.24 katika robo tatu za kwanza kuliko mwaka jana wakati kama huo, CAAM inasema.

Mauzo katika kipindi hicho hicho yalipanda kwa asilimia 34.9 na kufikia magari karibu milioni 11.23, yakichukua asilimia 46.1 ya jumla ya mauzo yote ya magari nchini China, takwimu hizo za CAAM zinaonyesha.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, sekta ya magari ya China ilidumisha uzalishaji na mauzo thabiti katika kipindi hicho, ikichochewa na mpango wa kubadilisha magari ya zamani kuwa magari mapya, maonyesho ya magari, na uzinduzi wa bidhaa mpya.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, uzalishaji wa jumla wa magari ulifikia magari milioni 24.33 katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13.3, wakati mauzo yaliongezeka kwa asilimia 12.9 kufikia magari milioni 24.36.

Takwimu hizo zilizotolewa Jumanne pia zinaonyesha kuwa mauzo ya nje ya China ya magari yaliendelea kuongezeka, yakiwa na ongezeko la asilimia 14.8 la mwaka. Hasa, yale ya NEV yaliongezeka kwa asilimia 89.4 kufikia magari milioni 1.76.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha