

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa Ufaransa Lecornu atangaza baraza jipya la mawaziri
![]() |
Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu akiondoka baada ya mkutano wa kwanza wa kila wiki wa baraza la mawaziri la serikali mpya katika Ikulu ya Elysee mjini Paris, Ufaransa, Oktoba 14, 2025. (Xinhua/Gao Jing) |
PARIS - Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu Jumapili jioni alitangaza serikali yake mpya, inayojumuisha jumla ya mawaziri 34, Ikulu ya Rais wa Ufarasa, Elysee imesema katika taarifa yake.
Mawaziri muhimu walioteuliwa, ni pamoja na Laurent Nunez kuwa waziri wa mambo ya ndani, Jean-Pierre Farandou waziri wa kazi, Monique Barbut waziri wa mageuzi ya muundo wa ikolojia, Edouard Geffray kuwa waziri wa elimu ya kitaifa, na Catherine Vautrin kuwa waziri wa ulinzi.
Roland Lescure ameteuliwa tena kuwa waziri wa fedha. Jean-Noel Barrot anaendelea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, huku Gerald Darmanin akibaki na wadhifa wake katika Wizara ya Sheria.
Lecornu alikutana na Rais Emmanuel Macron katika Ikulu ya Elysee mapema jioni, kwa mujibu wa habari za vyombo vya habari vya nchini humo. Lecornu alipendekeza "mchanganyiko wa viongozi wa mashirika ya kiraia wenye uzoefu na wabunge vijana" kwa baraza la pili la serikali yake.
Awali Lecornu alijiuzulu siku ya Jumatatu wiki iliyopita, chini ya mwezi mmoja baada ya uteuzi wake wa kwanza na siku moja tu baada ya kutangaza sehemu ya baraza lake la mawaziri la kwanza. Aliteuliwa tena kuwa waziri mkuu Ijumaa ya wiki hiyohiyo huku kukiwa na mvutano wa kisiasa unaoendelea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma