

Lugha Nyingine
Rais wa Madagascar aeleza kuwa "mahali salama" wakati kukiwa na maandamano yenye ghasia
Picha hii iliyopigwa kwenye skrini ikimuonyesha Rais wa Madagascar Andry Rajoelina akizungumza katika video iliyotolewa kwenye mtandao wa kijamii, Oktoba 13, 2025. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)
ANTANANARIVO - Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amesema kwamba amekimbilia "mahali salama" ili kuhakikisha usalama wake baada ya jaribio la mauaji dhidi yake ambapo katika video iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii, Rajoelina amedai kuwa alikuwa mlengwa wa jaribio la mauaji lililopangwa na "wanajeshi waliochochewa na wanasiasa."
Rajoelina hakudokeza mahali alipo lakini amesema kuwa njia pekee ya kutoka kwenye msukosuko unaoendelea nchini Madagascar ni kuheshimu Katiba ya Nchi.
Septemba 25, vijana wengi walianza kufanya maandamano kupinga ukosefu wa maji na umeme. Baadhi ya maandamano yalibadilika kuwa vurugu, na punde yalifikia hadi kutoa wito wa kumtaka rais ajiuzulu.
Oktoba 6, Rajoelina alimteua Ruphin Fortunat Dimbisoa Zafisambo kuwa waziri mkuu, wiki moja baada ya kuvunja serikali huku kukiwa na maandamano makubwa nchini kote.
Kwenye video hiyo ya Jumatatu, Rajoelina alisema kwa sasa "yuko kwenye jukumu" la kutafuta jenereta zitakazopelekwa kwa Madagascar kutatua tatizo la umeme la nchi hiyo.
"Sasa tutapokea jenereta, zilizotolewa na nchi marafiki," amesema Rajoelina, akiuhakikishia umma kwamba jenereta zitakazoletwa zitaziba vya kutosha nakisi ya megawati 58 iliyokadiriwa "katika miezi kadhaa ijayo."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma