

Lugha Nyingine
Kufungwa kwa serikali ya Marekani kwafikia siku ya 16 huku mvutano kati ya vyama viwili ukiendelea
Picha hii iliyopigwa Oktoba 12, 2025 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)
WASHINGTON – Kufungwa kwa sehemu kwa serikali ya Marekani kumefikia siku ya 16 leo Alhamisi, bila dalili za kufikia mwisho ambapo suala kuu ni msuguano kati ya wabunge wa vyama vya Democrats na Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani juu ya fedha za huduma ya afya, na hakuna upande ulio tayari kulegeza msimamo.
Bunge la Seneti juzi Jumanne lilikataa mswada wa bajeti ya muda mfupi uliopitishwa na Kambi ya Wabunge wa Republican ili kuifungua serikali kwa mara ya nane, ikihakikisha kufungwa kwa serikali kuingia wiki yake ya tatu. Mswada huo ulihitaji kura 60 ili kupitishwa na kusonga mbele lakini ulipata kura 49 pekee.
Spika wa Bunge la Marekani Mike Johnson, Mbunge wa Republican kutoka Jimbo la Louisiana, ameonya juu ya athari zinazowezekana kutokea za kufunga serikali kwa muda mrefu.
"Tunakabiliwa kuelekea moja ya ufungaji wa serikali wa muda mrefu zaidi katika historia ya Marekani, isipokuwa kama Wabunge wa Republican wataacha madai yao na kupitisha bajeti safi, isiyo na masharti ili kufungua tena serikali na kulipa wafanyakazi wetu wa serikali kuu," alisema Jumatatu.
Wabunge wa chama cha Democrat, kwa upande wao, wanawashutumu wenzao wa Republican kwa kutaka kupunguza bajeti muhimu ya afya kwa watu wa Marekani.
Kufungwa kwa muda mrefu zaidi kwa serikali ya Marekani kuwahi kurekodiwa kulichukua siku 35 wakati wa muhula wa kwanza wa Rais Donald Trump, mwishoni mwa 2018 na mapema 2019.
Wabunge wa Chama cha Republican wa Baraza la Wawakilishi wanadai kwamba wenzao wa Democrat wanataka kuongeza muda kufungwa kwa serikali kupita siku ya maandamano yaliyopangwa mwishoni mwa wiki hii mjini Washington, katika jaribio la kuwaonyesha wanaharakati wa chama hicho kwamba wanakabiliana dhidi ya utawala wa Trump.
Wafanyakazi zaidi ya 4,000 wa serikali kuu walipokea notisi za kuachishwa kazi, kwa mujibu wa kesi iliyofunguliwa mahakamani Ijumaa iliyopita. Ikulu ya White House Jumatatu wiki hii ilisema utawala unapanga kuendelea kufukuza kwa wingi nguvu kazi ya serikali kuu wakati kufungwa kwa serikali kukiendelea.
Msomi Mshiriki wa Taasisi ya Brookings Darrell West ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa: "Kufungwa kwa serikali kunaanza kuathiri uchumi na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi. Pia kunachelewesha uchapishaji wa ripoti muhimu za serikali."
"Kufungwa kwa serikali kunadhoofisha maoni ya kimataifa kuhusu Marekani na kuifanya ionekane kama viongozi wetu hawana uwezo. Mataifa mengine yatajenga hoja kuwa Marekani haijui namna ya kujitawala," West amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma