Vigezo vya China vyaimarisha juhudi za kutokomeza ugonjwa wa kichocho visiwani Zanzibar, Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2025

Mtaalamu wa afya kutoka China akionyesha  ufundi wa kuthibitisha ugonjwa wa kichocho kwa wataalamu wa afya wa Zanzibari kwenye warsha ya mafunzo visiwani Zanzibar, Tanzania, Oktoba 14, 2025. (Timu ya wataalamu wa China/kupitia Xinhua)

Mtaalamu wa afya kutoka China akionyesha ufundi wa kuthibitisha ugonjwa wa kichocho kwa wataalamu wa afya wa Zanzibari kwenye warsha ya mafunzo visiwani Zanzibar, Tanzania, Oktoba 14, 2025. (Timu ya wataalamu wa China/kupitia Xinhua)

DAR ES SALAAM - Wataalamu wa afya kutoka China wanaisaidia Zanzibar ya Tanzania kutokomeza ugonjwa wa kichocho kupitia kazi ya kueneza vigezo vya China vya kinga na udhibiti wa ugonjwa, na ufundi wa kuthibitisha ugonjwa.

Katika wakati wa maadhimisho ya 56 ya Siku ya Vigezo vya Dunia timu ya wataalamu wa China ya mradi wa kudhibiti ugonjwa wa kichocho visiwani Zanzibar juzi Jumanne ilifanya warsha ya kuongeza juhudi za kueneza vigezo vya China vya kudhibiti ugonjwa wa kichocho.

Warsha hiyo iliwakutanisha wataalamu weledi zaidi ya 60 kutoka idara za afya za Zanzibar, ambapo wataalamu wa China walielezea vigezo muhimu vya kitaifa vinavyotokana na uzoefu wa mafanikio wa China katika kudhibiti ugonjwa wa kichocho.

Vigezo hivyo vikiwemo vigezo vya usimamizi wa mgonjwa, mbinu za upimaji kwa kutumia hadubini ya kuchuja mkojo, upimaji wa asidi ya nukleiki kupitia uongezaji joto (isothermal amplification) unaosaidiwa na recombinase, na vigezo vya udhibiti wa konokono kupitia matumizi ya molluscicide.

Wataalamu wa China walieleza kwa kina mchakato mzima wa kazi zinazofuata vigezo za kuripoti tatizo la afya, upimaji wa kimaabara, udhibiti wa konokono, na kurekodi matokeo, wakisisitiza kwamba taratibu za kufuata vigezo ni muhimu kwa kuboresha usahihi wa kuthibitisha ugonjwa na ufanisi wa kufanya matibabu.

Wang Wei, kiongozi wa timu hiyo ya wataalamu wa China, amesema warsha hiyo imewafanya wafanyakazi wa afya wenyeji kuelewa zaidi kuhusu vigezo vya udhibiti wa ugonjwa wa kichocho na kuwapa ujuzi wa kuthibitisha ugonjwa, kuimarisha uwezo wa Zanzibar katika ufuatiliaji, uthibitishaji na uzuiaji wa magonjwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha