Wizara ya Ulinzi ya China yalaani Marekani kuiuzia silaha Taiwan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2025

BEIJING - Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya China imelaani Marekani kutangaza hivi karibuni kwamba itaiuzia Taiwan silaha zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 330, wizara hiyo ya China ikiapa kuchukua hatua zote za lazima ili kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi.

Akijibu swali la vyombo vya habari jana Jumatatu, msemaji wa wizara hiyo Zhang Xiaogang amesema uuzaji huo wa silaha unakiuka vibaya kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, unaingilia kijeuri kati ya mambo ya ndani ya China, kudhuru mamlaka ya nchi na maslahi ya usalama ya China, na kutoa ishara mbaya sana kwa nguvu ya mafarakano ya kutaka “Taiwan Ijitenge”.

"Tunalaumu vikali na kupinga kithabiti juu ya vitendo hivyo na tumetoa malalamiko mazito kwa upande wa Marekani," Zhang amesema.

Zhang amesema kwamba jaribio lolote la kusaidia "Taiwan Ijitenge" kwa mbinu za kijeshi litaleta matatizo tu kwake yenyewe, na jaribio la "kutumia Taiwan kuizuia China" hakika litashindwa.

"Tunahimiza upande wa Marekani kuacha mara moja vitendo vyake vya makosa vya kuipa Taiwan silaha ili kuepuka kuathiri maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na uhusiano wa majeshi ya pande hizo mbili," amesema.

"Pia tunauonya utawala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwamba kutumia vibaya pesa za watu katika eneo la Taiwan zilizopatikana kwa shida kununua silaha kutaweza tu kuelekea siku yake ya mwisho, na jaribio lolote la kutafuta kujitenga kwa kutegemea nguvu za nje au kususia muungano wa taifa kwa silaha hakika litashindwa," ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha