Waziri Mkuu wa China aahidi kuimarisha zaidi ushirikiano na Russia katika uwekezaji, nishati na kilimo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin mjini Moscow, Russia, Novemba 17, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin mjini Moscow, Russia, Novemba 17, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

MOSCOW - Waziri Mkuu wa China Li Qiang kwenye mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin mjini Moscow jana Jumatatu amesema kwamba China inapenda kuimarisha ushirikiano na Russia katika uwekezaji, nishati, kilimo na maeneo mengine, akiongeza kuwa soko la China linakaribisha bidhaa zenye sifa bora za kilimo na vyakula zaidi kutoka Russia.

Li amesema kwamba hivi karibuni yeye na Mishustin walifanya mkutano wa 30 wa kawaida wa wakuu wa serikali za China na Russia mjini Hangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, ambao ulisisitiza utekelezaji wa makubaliano muhimu yaliyofikiwa na Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin.

Amesema, mkutano huo, pia ulipitia kwa kina maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Russia katika sekta mbalimbali na kuweka mipango juu ya ushirikiano muhimu katika hatua inayofuata.

China ina nia ya kushirikiana na Russia kufuata mwongozo wa kimkakati wa wakuu hao wa nchi mbili, kuimarisha zaidi mawasiliano, kuendelea kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande hizo mbili.

Li ameelezea matumaini yake kwamba upande wa Russia utatoa urahisi zaidi kwa kampuni za China kuwekeza na kufanya biashara zao nchini Russia.

Amehimiza kusukuma mbele zaidi ushirikiano wa kivitendo ili kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), kuboresha ujenzi wa mifumo ya SCO, kuongeza ushawishi wake katika masuala ya kimataifa, na kushikilia katika mshikamano na idadi kubwa ya nchi za Kusini ili kuhimiza dunia yenye ncha nyingi na yenye usawa na utaratibu na kukuza utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa kwa wote na jumuishi.

Kwa upande wake Mishustin amesema kwamba kwa sasa, ushirikiano wa kimkakati wa uratibu wa pande zote katika zama mpya kati ya Russia na China uko katika ngazi ya juu ambayo haijawahi kutokea.

"Russia inataka kuongeza zaidi mazungumzo na mawasiliano na China katika ngazi zote, kuzidisha ushirikiano katika uchumi na biashara, nishati, kilimo, na mawasiliano ya watu na utamaduni, kuanzisha maeneo mapya ya ukuaji kwa ajili ya ushirikiano, na kuimarisha urafiki wa ujirani mwema," ameongeza.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin mjini Moscow, Russia, Novemba 17, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin mjini Moscow, Russia, Novemba 17, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha