Lugha Nyingine
China na Ujerumani zafanya mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya mambo ya fedha mjini Beijing

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng akiongoza mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya mambo ya fedha kati ya China na Ujerumani kwa pamoja na Naibu Chansela ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Serikali Kuu ya Ujerumani Lars Klingbeil mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 17, 2025. (Xinhua/Dai Tianfang)
BEIJING – Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng ameongoza mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya mambo ya fedha kati ya China na Ujerumani kwa pamoja na Naibu Chansela ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Serikali Kuu ya Ujerumani Lars Klingbeil mjini Beijing jana Jumatatu, huku pande zote mbili zikikubaliana juu ya mambo mbalimbali yenye matokeo ya kunufaishana.
Naibu Waziri Mkuu He, ambaye aliongoza ujumbe wa China kwenye mazungumzo hayo, amesema kwamba China ina nia ya kushirikiana na Ujerumani ili kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango mpya katika utulivu na ukuaji wa uchumi duniani.
Kwa upande wake Klingbeil, ambaye aliongoza ujumbe wa Ujerumani, amesema kwamba Ujerumani ina nia ya kushiriki kwenye mawasiliano na ushirikiano wa karibu na China katika sekta ya mambo ya fedha na sarafu, kwa lengo la kuhimiza maendeleo makubwa zaidi kwenye uhusiano wa pande mbili.
He na Klingbeil pia walihudhuria Majadiliano ya pili ya Mambo ya Fedha kati ya China na Ujerumani.

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng akiongoza mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya mambo ya fedha kati ya China na Ujerumani kwa pamoja na Naibu Chansela ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Serikali Kuu ya Ujerumani Lars Klingbeil mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 17, 2025. (Xinhua/Dai Tianfang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma